Millionaire  Ads

RATIBA VPL 15/10/2016


Michezo mitatu ya ligi kuu Tanzania bara kupigwa leo hii mchezo namba 73 utazikutanisha simba na kagera sugar katika dimba la uwanja wa uhuru jiji Dar es salaam kuanzia saa kumi kamili kwa saa za afrika mashariki. ligi hiyo inayoshirikisha timu 16 simba ndio kinara wa ligi hiyo ikiwa mbeleya stand united ya shinyanga kwa pointi moja. mchezo huo utasimamiwa na Hussein Athuman kutoka mkoani Katavi ambako pembeni atasaidiwa na Joseph Bulali wa Tanga na Silvester Mwanga wa mkoani Kilimanjaro wakati Soud Lila wa Dar es Salaam atakuwa mwamuzi wa akiba huku Kamishna wa mchezo akiwa Pius Mashera wa Dodoma.
michezo mingine ni mchezo namba 74 kati yaJKT Ruvu na Mwadui ya Shinyanga utakao fanyika mkoani pwani katika dimba la mabatini mchezo huo utasimamiwa na Mwanamama mwamzi mwenye beji la FIFA, Mwanahamisi Matiku wa Dar es Salaam, akisaidiwa na Shafii Mohamed pia wa Dar es Salaam na Gesper Ketto wa Arusha.
mchezo mwingine ni huko mkoani shinyanga ambapo vijana wanaoonekana wamezamiria kufanya makubwa msimu huu standa united wanaoshika nafasi ya pili nyuma ya simba wataikaribisha African Lyon kwenye Uwanja wa CCM Kambara kattika mchezo namba 75 utakaochezeshwa na Eric Onoka wa Arusha akisaidiwa na Agnes Pantaleo pia wa Arusha na Omary Juma wa Dodoma, mwamuzi wa akiba atakuwa Joseph Pombe wa Shinyanga, Kamishna wa mchezo atakuwa Hamisi Kitila wa Singida.

Millionaire  Ads

Share :

Facebook Twitter Google+ Lintasme

Related Post:

0 Comment untuk "RATIBA VPL 15/10/2016 "

Back To Top