Millionaire  Ads

RATIBA MICHUANO YA LIGI YA MABINGWA BARANI ULAYA LEO USIKU 22/11/2016



Michezo nane ya makundi manne kundi(E - h) kupigwa leo katika viwanja mbalimbali barani ulaya .

Kundi E kutafanyika mchezo wa mapema zaidi kati ya wenyeji CSKA Moscow watakapoikaribisha  Bayer Leverkusen mchezo utakaofanyika 20:00 EAT.

Mchezo mwingine wa kundi E ni kati ya Monaco na Tottenham Hotspur mtanange utakaopigwa saa 22:45 .

Michezo mingine ni kundi F wakati timu ambayo msimu huu imepania kufanya maajabu Borussia Dortmund wataikaribisha Legia Warszawa katika mchezo wa hatua ya 5 huku Borussia Dortmund wakiwa vinara wa kundi hilo wakifuatiwa kwa karibu na Real Madrid, Borussia wana pointi 10 huku madrid wakiwa na pointi 8.
Mchezo mwingine ni kati ya Sporting CP na Real Madrid

Kundi G michezo itakuwa kati FC Koebenhavn na FC Porto huku mchezo mwingine ukizikutanisha Leicester City na Club Brugge.


Kwenye kundi H wenyeji Sevilla wataikaribisha Juventus huku kila timu ikitaka kukata tiketi yake mapema ya robo fainal, Juventus ipo nyuma ya Sevilla kwa pointi 2, sevilla ina pointi 10, juve 8.

Mchezo mwingine ni kati ya Dinamo Zagreb watakapoikaribisha Lyon, huku Dinamo Zagreb wakikumbuka kipigo cha goli 3 bila majibu katika mchezo wake wa mwisho kutoka kwa Lyon.

Nb: Michezo yote hapo juu itaanza saa 22:45 EAT




Millionaire  Ads

Share :

Facebook Twitter Google+ Lintasme

Related Post:

0 Comment untuk "RATIBA MICHUANO YA LIGI YA MABINGWA BARANI ULAYA LEO USIKU 22/11/2016"

Back To Top