Timu ya taifa ya Uganda jana iliendelea kulitangaza soka la
Afrika mashariki vizuri baada ya kuifundisha soka timu ya taifa ya Congo kwa
kuichapa goli 1 bila majibu na kuweza kukamata usukani wa kundi E.
Ikicheza kwa kujiamini Uganda crane’s huku ikishangiliwa na
umati wa wapenda soka nchini Uganda iliwachukua takiribani dakika 18 baada ya mchezo
kuanza kujipatia bao hilo la pekee liliofunga na Farouk Miya .
Mchezo mwingine wa raundi ya 3 kufuzu kombe la dunia nchini Urusi 2018 Kundi E utapigwa leo katika nchi ya Misri
wakati mafarao wa Misri watakapoikaribisha timu ya Taifa ya Ghana mchezo
utakaoanza 1900 kwa saa za Afrika mashariki.
matokeo mengine ni kama yanavyoonekana:-
KUNDI B
Cameroon 1 - 1 Zambia
Nigeria 3 - 1 Algeria
KUNDI C
Mali 0 - 0 Gabon
Morocco 0 - 0 Ivory Coast
KUNDI D
South Africa 2 - 1 Senegal
Cape Verde 0 - 2 Burkina Faso
Millionaire Ads
0 Comment untuk "UGANDA CRAN'S WAENDELEA KUIBEBA AFRIKA MASHARIKI "