Michezo matatu ligi kuu Tanzania bara vpl kupigwa leo katika mikoa mitatu tofauti
Jijini Dar es Salaam
simba wataonyeshana ubabe
na wanalambalamba Azam fc katika mchezo ambao utakuwa ni mgumu na utabiri wake
hauelezeki,

Azam ambao raundi ya pili wamekifanyia maboresho makubwa kikosi
chao kuanzia benchi la ufundi mpaka wachezaji.
Simba wanaingia Uwanja wa taifa wakiwa na kumbukumbu ya kichapo
cha goli moja toka kwa Azam siku chache zilizopita katika mchezo wa finali
kombe la mapinduzi.
Tutarajie soka safi na lenye ushindani ikizingatiwa simba
inatafuta taji la vpl ambalo imeliasi kwa mudda mrefu wakati azam ikijaribu
kurejea katika nafasi ya tatu.
Jijini Mbeya
Kutakuwa na derby ya mkoa huo ambapo wajelajela Tanzania Prisons
watakipiga na ndugu zao wa Mbeya city.

Mkoani Mtwara
Ndanda wao watawakaribisha jiranizao Majimaji toka mjini songea
katika mchezo ambao utakuwa mkali hasa ukifutilia Matokeo mabovu kwa timu hizi
mbili msimu huu.

0 Comment untuk "simba vs Azam ni vita ya dakika 90"