kikosi cha yanga
Wakiwa ugenini
wawakilishi wa Tanzania bara katika ligi ya mabingwa barani Afrika timu ya
Yanga leo imefanya ilichotumwa na Taifa la Tanzania huko Comoro baada ya
kuishushia kipigo kikali cha goli 5 – 1 timu ya Ngaya FC ya Comoro.
Mabingwa hao
wa Tanzania walianza kufumania nyavu za wacomoro hao dakika 38 kupitia kwa Justin
Zullu.
Dakika chache
badae Simon Msuva aliipatia yanga goli la pili, mpka timu zinakwenda mapumziko
ubao ulikuwa unasomeka Ngaya 0 – 2 yanga.
Kipindi cha
pili dakika ya 58 Obrey Chirwa 59 alipachia goli la tatu, dakika sita badae
Mrundi Hamis Tambwe alishindilia msumari wa 4 kwenye jahazi la wacomoro.
Goli la
mwisho la yanga kwa siku ya leo limefungwa na Kamusoko katika 73’, wakati lile
la kufutia mazchozi la Ngaya lilifungwa na Anfane 66'.
Mpaka mpira
unamalizika Ngaya FC 1 – 5 Yanga SC .
Yanga watarejea
jijini Dar es salaam siku ya jumatano tayari kwa maandalizi ya mchezo wa
marudianona Ngaya FC utakaofanyika Uwanja wa taifa siku ya jumamosi February 18.
Millionaire Ads
0 Comment untuk "Ngaya FC 1 - 5 Young Africans SC, kilabu bingwa Afrika"