Muda: 22:45
Barcelona wanaikaribisha PSG katika
dimba la Camp Nou wakiwa na kumbukumbu ya kipigo kikali cha goli 4 – 0 walichokipata
February 14 mwaka huu.
Barcelona ndio vinara wa ligi kuu ya
Hispania kwa kujikusanyia pointi 60 baada ya michezo 26 mbele ya real Madrid
wenye pointi 59 baada ya michezo 25.
Baada ya kichapo hicho Barcelona
wanaonekana kujipanga upya na wamekuwa wakipata ushindi mkubwa hasa katika
michezo yao ya mwisho angalia rekodi hapo chini za laliga.
MICHEZO 5 YAMWISHO
YA BARCELONA
Barcelona 5-0 Celta Vigo Mar 4,
2017 LALIGA
Barcelona 6-1 Sporting Gijón Mar 1, 2017 LALIGA
Atletico Madrid 1-2 Barcelona Feb
26, 2017 LALIGA
Barcelona 2-1 Leganes Feb 19, 2017 LALIGA
Paris Saint-Germain 4-0 Barcelona
Feb 14, 2017 UEFA Champions League
PSG tangu waifunge Barcelona
hawajapoteza mchezo, wameshinda michezo mitatu na kutoka sare mchezo mmoja, Miongoni
mwa michezo hiyo ni ushindi mkubwa kabisa wa goli 5 – 1 ugenini dhidi ya
Marseille kwenye ligi kuu ya Ufaransa.
Tizama Matokeo ya PSG kwenye michezo
yake mitano ya mwisho .
MICHEZO 5 YA MWISHO
YA PSG
Paris Saint-Germain 1-0 AS Nancy, Mar
4, 2017 Ligue 1
Niort 0-2 Paris Saint-Germain Mar 1,
2017 LIGI
Marseille 1-5 Paris Saint-Germain
Feb 26, 2017 Ligue 1
Paris Saint-Germain 0-0 Toulouse Feb
19, 2017 Ligue 1
Paris Saint-Germain 4-0 Barcelona
Feb 14, 2017 UEFA Champions League
MICHEZO 5YA
MWISHO WALIYOKUTANA (Head To Head Record
)
Katika michezo mitano
iliyozikutanisha timu hizi mbili Barcelona imeshinda mara tatu na PSG
wameshinda mara mbili. Angalia Matokeo hapa chini.
Paris Saint-Germain 4-0 Barcelona
Feb 14, 2017 UEFA Champions League
Barcelona 2-0 Paris Saint-Germain
Apr 21, 2015 UEFA Champions League
Paris Saint-Germain 1-3 Barcelona
Apr 15, 2015 UEFA Champions League
Barcelona 3-1 Paris Saint-Germain
Dec 10, 2014 UEFA Champions League
Paris Saint-Germain 3-2 Barcelona
Sep 30, 2014 UEFA Champions League
Je kwa mtiririko huo hapo juu Barcelona itaweza kuifunga PSG
goli 5 – 0 ?.
Je PSG haitapata goli Camp Nou leo?
Toa maoni yako
Millionaire Ads
0 Comment untuk "Barcelona vs PSG, je Barcelona kushinda 5 - 0 ?"