Millionaire  Ads

ENGLAND: Liverpool Vs Arsenal, historia, uchambuzi na utabiri kabla ya mchezo wa march 4



MUDA: 20:30

UWANJA: ANFIELD,LIVERPOOL


Liverpool wanawaalika Arsenal katika dimba la Anfield wikiendi hii wakiwa na rekodi nzuri ya mechi mchezo wa kwanza uliofanyika Emirates ambapo walishinda 4 – 3 dhidi ya Arsenal kwa magoli ya Coutinho (45'+1, 56’), Lallana (49'), Mané (63') wakati yale ya Arsenal yalifungwa na Walcott (31'), Oxlade-Chamberlain (64'), Chambers (75').



Liverpool pia wanaingia uwanjani jumamosi wakiwa na kazi moja tu ya kuhakikisha wanashinda Kutokana na shinikizo la Manchester United ambayo inaonekana kuimarika ikiwa nyuma kwa alama 1 tu.

Mchezo wa mwisho wa Liverpool ilikubali kipigo kikali toka kwa bingwa mtetezi wa ligi hiyo Leicester City cha goli 3 – 1.

Mchezo wa jumamosi unakuwa na hamasa ya aina yake kwani timu hizo mbili zinapishana pointi moja tu Liverpool wanapointi 49 baada ya michezo 26 katika nafasi ya 5 huku Arsenal wakiwa na pointi 50 katika michezo 25.

Liverpool na Arsenal tangu mwaka 2010 wamekutana mara 13, Arsenal wameshinda mara nyingi zaidi mara 4 wakati Liverpool wameshinda mara 3 na kutoka suluhu mara 6.

Jumla ya magoli 45 yamefungwa katika michezo hiyo na vipigo vikubwa ni 08 Feb 2014 Liverpool 5 Arsenal 1 katika dimba la Anfield.

04 Apr 2015 Arsenal 4 Liverpool 1katika dimba la Emirates.

Zifuatazo ni rekodi za Liverpool na Arsenal katika ligi kuu tangu 2010

15 Aug 2010   Liverpool v Arsenal    1-1        2010/2011

17 Apr 2011    Arsenal v Liverpool    1-1       

20 Aug 2011   Arsenal v Liverpool    0-2       2011/2012

03 Mar 2012    Liverpool v Arsenal    1-2       

02 Sep 2012    Liverpool v Arsenal    0-2       2012/2013

30 Jan 2013     Arsenal v Liverpool    2-2       

02 Nov 2013   Arsenal v Liverpool    2-0       2013/2014

08 Feb 2014    Liverpool v Arsenal    5-1       

21 Dec 2014    Liverpool v Arsenal    2-2       2014/2015

04 Apr 2015    Arsenal v Liverpool    4-1       

24 Aug 2015   Arsenal v Liverpool    0-0       2015/2016

13 Jan 2016     Liverpool v Arsenal    3-3      

14 Aug 2016   Arsenal v Liverpool    3-4       2016/2017


4 March 2017  Liverpool vs Arsenal      ?         
Millionaire  Ads

Share :

Facebook Twitter Google+ Lintasme

Related Post:

0 Comment untuk "ENGLAND: Liverpool Vs Arsenal, historia, uchambuzi na utabiri kabla ya mchezo wa march 4"

Back To Top