Millionaire  Ads

Leicester City vs Sevilla, Mahrez na Samir Nasr nani fundi wa kuchezea mpira



Leicester City na Sevilla leo saa 22:45 ni vita isiyotabirika kiurahisi hasa ukiingalia Sevila inafaida ya goli moja katika ushindi wa 2 - 1 nyumbani kwake.

Leicester chini ya kocha wao wa muda Craig Shakespeare wamefanya vizuri michezo yao ya hivi karibuni katika ligi kuu ya Uingereza

leo tunategemea kuona Leicester City wakianza kwa kushambulia ili kupata goli na kujitengenezea mazi ngira mazuri ya kuweka rekodi nyingine kubwa kwa kilabu hiyo baada ya ile ya kutwaa EPL.

leo tutegemee kuona mpira wa ufundi mwingi kutoka kwa Mahrez kwa upande wa Leicester City na Samir Nasr kwa upande wa Sevila.

mchezo mwingine ni kati ya Juventus ya Italia watakabiliana FC Porto ya Ureno katika mchezo mwingine ambao Juve anapewa nafasi kubwa ya kushinda kutoka na uzoefu na mwenendo wake kwenye michezo yake ya hivi karibuni

mchezo wa kwanza uliofanyika Ureno Porto walikubali kipigo cha goli 2 - 0 dhidi ya Juventus tarehe 22/2/2017

Je Porto atapindua matokeo na kuishangaza dunia tusubiri saa 22:45 usiku.

Millionaire  Ads

Share :

Facebook Twitter Google+ Lintasme

Related Post:

0 Comment untuk "Leicester City vs Sevilla, Mahrez na Samir Nasr nani fundi wa kuchezea mpira"

Back To Top