Michael Owen na Martin Keown waweka
hadharani utabiri wao Tottenham vs Everton
Mchezaji wa zamani wa Manchester
United Michael Owen ameitabiria ushindi tottenham dhidi ya Everton katika dimba la White
Hart Lane.
Owen alisema “namwaangalia Harry
Kane na Romelu Lukaku naona magoli
kutoka kwao lakini mwenyeji atashinda mchezo huu”
Utabiri wa Owen ni kuwa timu zote
zitapata magoli lakini Tottenham watashinda mchezo huo. Owen aliandika kwenye Betvictor.com.
Kwa upande wa mchezaji wa dhamani wa
arsenal Martin Keown alikaririwa na gazeti la Daily Mail akizungumzia mchezo wa
leo kwa kusema “Tottenham wapo vizuri na kuwa nyumbani kutawaongezea nguvu”.
“si kazi ndogo kuishinda Everton
lakini nasema Matokeo yatakuwa 2 - 1”.
Millionaire Ads
0 Comment untuk "Michael Owen na Martin Keown waipa ushindi Tottenham"