Kocha mkuu wa timu ya Atletico Madrid
amewaambia Washabiki wa timu hiyo na wachezaji wake kuwa anaamini bado timu
yake inanafasi ya kutinga fainali ya ligi ya Mabingwa barani ulaya.
Kwa mujibu wa jarida maarufu la michezo
la nchini Hispania Marca, Simeone alisema “I say to my players and fans that a
comeback is possible”
Usiku wa may 2 Atletico Madrid
ilikubali kipigo kikali toka kwa mahasimu zao wa mji mmoja timu ya Real Madrid,
Real Madrid iliichapa Atletico Madrid
3 – 0 magoli yote yalipachikwa kimiani na mchezaji bora wa dunia C. Ronaldo.
Wakati huo huo mtifuano wa kuwania
kiatu cha dhahabu cha kilabu bingwa ulaya unaelekea kumuendea vizuri Ronaldo
baada ya kufikisha magoli 10 nyuma ya Messi mwenye magoli 11 wakati Ronaldo bado
anaendelea na mashindano.
matokeo ya mchezo wa pili nusu fainali ligi ya mabingwa ulaya monaco 0 - 2 juventus magoli yote yamefungwa na Gonzalo Higuain 29' na 59'.
matokeo nusufainali ya kwanza Europa ligi Ajax 4 - 1 Lyon.
leo ni Celta Vigo vs Manchester United 22:05 katika nusu fainali ya pili ya europa.
0 Comment untuk " Diego Simeone anaamini maajabu yanaweza kutokea mechi ya mrudiano,Ronaldo akaribia kiatu cha dhahabu, Juve yanusa fainali"