Serengeti boys waanza na sare na bingwa mtetezi
Afcon U17 Gabon
Timu ya Taifa ya Tanzania chini ya umri wa miaka 17
Serengeti Boys leo imegawana pointi na bingwa mtetezi wa michuano hiyo timu ya
taifa ya Mali.
Mali walionekana wazuri zaidi kipindi cha kwanza na
kuutawala mchezo kwa asilimia kubwa huku Serengeti Boys wakifanya kazi kubwa
kulinda goli lisiingie.
Kipindi cha pili Serengeti Boys waligeuza mchezo na
kuwaduwazaa mali na kushindwa kuamini kuwa Serengeti ndio wale wa kipindi cha
kwanza au wengine, waliutawala mpira vizuri hasa eneo la kati ambapo kiungo
Kelvin Naftal alifanya anavyotaka.
Hadi mwisho wa mchezo wenyeji Mali 0 – 0 Tanzania.
Hii inamaana kuwa Tanzania wanahitaji ushindi katika
timu zilizosalia ili waweze kufuzu kwa kombe la dunia nchini India.
Kilalakheri Tanzania kilalakheri Serengeti Boys.
0 Comment untuk "Mali 0 - 0 Tanzania, AFCONU17 Gabon, Serengeti wazidi kuweka rekodi Afrika"