Bodi ya ligi nchini ‘TANZANIA PREMIER LEAGUE BOARDS(TPLB)’
jana imeshindilia kaa la moto katika maamuzi yake ya kipoka timu ya Kagera
Sugar pointi 3 na magoli 3 kwa kosa la kumchezesha mchezaji Mohamed Fakhi kwa
kusema Fakhi wakati anaichezea Kagera Sugar hakuwa na kadi tatu za njano.
Vionjo vilivyo kwenye Barua hiyo ni kama ifuatavyo ”TFF
ndio yenye dhamana ya usimamizi wa mpira nchini na ambayo ndio iliyokasimu
madaraka kwa TPLB kuendesha ligi kuu” barua iliiendelea kwa sema “baada ya
uchunguzi wao ambao ulihoji watu mbalimbali wamebaini kuwa mchezaji Mohamed
Fakhi alielalamikiwa na Simba hakuwa na kadi 3 za njano siku ya mchezo wa
Kagera sugar na Simba, kwa mantiki hiyo maamuzi yaliyofanywa na kamati ya
kuipoka pointi Kagera hayakuwa sahihi na hivyo Matokeo ya uwanjani ambayo
yalikuwa ni ushindi wa 2 – 1 kwa Kagera sugar yabaki kama yalivyo.”
Barua hiyo pia imeiruhusu simba kukata rufaa huku
ikifuata taratibu za mchezo wa soka.
Kwa mantiki hiyo simba imepewa rungu la kuingilia
FIFA.
0 Comment untuk " Safari ya Simba kuishtaki TFF FIFA imeiva ni baada ya jana kupewa barua yao rasmi ya kupokwa pointi 3 na bodi ys ligi."