Kocha
wa Serengeti Boys Bakari Shime ameiambia Cafonline endapo atafudhu kwenda kombe
la Dunia ni mafanikio makubwa kwake na Taifa ila amewatoa hofu wa Tanzania
endapo atafudhu kombe la dunia,”Mwaka jana nilialikwa kwenye michezo kabla ya
kombe la dunia’Pre world cup’ na tulicheza na USA, South Korea, Malaysia,
tunauzoefu kidogo na nina Imani tutaiwakilisha vyema Afrika kwenye michuano
hiyo” alisema Shime.
Katika
mchezo wa leo Serengeti Boys wanahitaji sare ili waweze kutinga hatua ya nusu
fainali na kupata tiketi ya kuliwakilisha Bara la Afrika kwenye kombe la Dunia.”kitu
muhimu kwetu ni kucheza nusu fainali na kupata tiketi ya kombe la Dunia nchini
India, Tunatambua Niger ni timu ngumu lakini tunakwenda kupigana walau tupate
pointi 1 au tatu ili tufanikiwe katika ndoto zetu” Shime aliliambia Cafonline.
Serengeti
boys leo inashuka dimbani kwa lengo moja tu la kusaka sare au ushindi ili
kusonga mbele.
Watanzania wote na wana Afrika mashariki shime tuiombee dua
timu yetu ya Tanzania
Mungu ibariki Serengeti Boys
Mungu ibariki Tanzania
Millionaire Ads
0 Comment untuk "TanzaniaU17 vs NigerU17, Rekodi, Ratiba, Shime aitangazia kiama Niger, nia yake ni kucheza kombe la dunia kwani alishawahi kualikwa maandalizi kombe hilo mwaka jana huko India."