Mshambuliaji hatari wa Simba na timu
ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars Ibrahim Ajib Migomba amesaini kandarasi ya
miaka miwili kuitumikia timu ya Yanga.
Hayo yalinukuliwa na waandishi wa
habari baada ya kukihoji Chanzo cha ndani cha timu ya Yanga ambacho kilikiri
kumpa mkataba mchezaji huyo.
Akihojiwa na EFM radio ya jijini Dar
es salaam jana alhamisi june 15, Kaburu alisita kukubali au kukanusha taarifa
hizo kwa kudai kuwa wakuulizwa na mchezaji husika ndie anaejua ukweli ulivyo “sisi
tumempa ofa yetu hajasaini na Simba inautaratibu wake hatuwezi kumlazimisha
mchezaji” alisema Kaburu, “ukitakata kujua kama kasaini yanga muulize mwenyewe
atakuwa na majibu” Kaburu aliongeza.
Alipoulizwa katibu mkuu wa Yanga
Mkwasa yeye alisema wao wapo kimya kimya taarifa zitawajia punde na kuhusu
ukata ndani ya kilabu hiyo alisisitiza kuwa timu sasa ipo vizuri na haina ukata
tena.
Inasadikiwa katika mkataba wa Ajib amepewa nyumba na gari la kutembelea.
Millionaire Ads
0 Comment untuk "Ajib rasmi yanga miaka miwili,kaburu asita kutoa majibu"