Ronaldo aendelea kuweka rekodi Ulaya
goli mbili ni rekodi mpya kwake
Licha ya kutwaa kiatu cha dhahabu
katika mazingira ambayo Hakuna alitegemea CR7 jana aliingia kwenye kitabu cha
kumbukumbu cha wachezaji wachache waliofunga magoli mawili katika mchezo wa
fainali wa kombe hilo akiungana na Daniele Massaro (Milan 1994), Karl-Heinz
Riedle (Borussia Dortmund 1997), Hernán Crespo (Milan 2005), Filippo Inzaghi
(Milan 2007) and Diego Milito (Internazionale 2010).
Ikumbukwe kuwa Hakuna mchezaji
yoyote ambae amewahi kufunga goli tatu katika mchezo wa fainali.
CR7 jana aliisaidia Real Madrid
kutwaa kikombe cha pili mfululizo katika michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya
baada ya kufunga magoli mawili na mawili wakigawana Casemiro na Marco Asensio.
Ronaldo licha ya kutwaa kiatu cha
dhahabu yeye ndie mfungaji mwenye magoli mengi kwa msimu mmoja alifanya hivyo
msimu wa 2014/15 alifunga goli 17.
CR7 ndie mwenye rekodi ya kufunga
magoli mengi katika hatua ya makundi alifunga goli 11 msimu wa 2014/15. Messi anafuata
kwa kufunga goli 10 katika makundi.
CR7 ndie anaeongoza kuwa na magoli
mengi katika historia ya ligi ya mabingwa amefunga magoli 105 baada ya kucheza
michezo 140 akifuatiwa na messi mwenye magoli 94 baada ya kucheza michezo 115.
0 Comment untuk "Ronaldo aendelea kuweka rekodi Ulaya goli mbili ni rekodi mpya kwake, ampiku Messi kimaajabu"