Rais wa shirikisho la
miguu nchini Tanzania Jamali Malinzi na katibu wake Celestine Mwesigwa Pamoja na
mhasibu wa TFF Isinde Isawafo Mwanga kwa mara ya pili leo wamerudishwa tena lupango
baada ya ushahidi unaowakabili
kutokamilika.
Watatu hao leo
walipandishwa kizimbani na kusomewa mashtaka yao katika mahakama yahakimu mkazi
Kisutu.
Baada ya kusomewa
mashitaka yao kesi yao imepelekwa mbele hadi july 30 mwaka huu itakapotajwa
tena.
Wamesomewa mashitaka 28 ya
kughushi na kutakatisha fedha kupitia akaunti ya TFF iliyopo katika banki ya
Stanbic, Dar es Salaam.
Malinzi aliingia
madarakani 2013 baada ya kumshinda mpinzani wake Athumani Nyamlani.
Uchaguzi huu haumhusu
Malinzi tena baada ya kukosa sifa za kugombea Kutokana na kutofanyiwa ‘interview’
Uchaguzi mkuu utafanyika
August 12 mwaka huukatikati ya nchi Dodoma
0 Comment untuk "MALINZI, MWESIGWA MAMBO MAGUMU WARUDISHWA TENA RUMANDE"