Chelsea wabanwa mbavu darajani, Man
U wakaribia 16 Bora
Timu ya Chelsea ya London Uingereza
jana ikiwa ndani ya Uwanja wake wa nyumbani imekubali sare ya goli 3 – 3 na
timu ya AS Roma ya Italia.
Chelsea ndio waliotangulia kutikisa
nyavu za wapinzani mara mbili katika kipindi cha kwanza na washaiki wakajua
lazima Chelsea ingeondoka na lundo la magoli.
Ilikuwa ni dakika ya 11 ambapo David
Luiz aliipatia uongozi Chelsea, na dakika ya 37 Eden Hazard aliipatia Chelsea goli
la pili, AS Roma walijiuliza na dakika ya 40 Aleksandar Kolarov aliipatia AS
Roma goli kwanza.
Mpaka kipindi cha kwanza
kinamalizika Chelsea 2 – 1 AS Roma.
Kipindi cha pili AS Roma walionekana
bora zaidi na dakika ya 64 Edin Dzeko aliisawazishia timu yake baada ya kazi
safi ya Federico Fazio.
Kasi ya AS Roma ilizaa matunda baada
ya Dzeko tena kuifungia timu yake goli la tatu na kuisadia timu yake kuiongoza
Chelsea hadi dakika ya 75 ambapo Eden Hazard aliisawazishia Chelsea.
Mpaka mpira unamalizika Chelsea 3 –
3 AS Roma.
Kitu kizuri kwenye mchezo wa jana ni
kuwa na kadi moja tu njano kwa dakika zote 90 na kadi hiyo alipewa mchezaji wa
Chelsea Tiemoue Bakayoko
Matokeo mengine ya ligi ya maingwa
Barani Ulaya usiku wa kuamkia leo:
KUNDI A:
Benfica 0 - 1 Manchester United (Marcus
Rashford 64’)
CSKA Moscow 0 - 2 Basel (Taulant
Xhaka 29’, Dimitri Oberlin)
KUNDI B:
Anderlecht 0 - 4 Paris Saint Germain
(Kylian Mbappe 3’, Edinson Cavani 44’, Neymar 66’, Angel Di Maria 88’)
Bayern Munich 3 - 0 Celtic (Thomas
Mueller 17’, Joshua Kimmich29’, Mats Hummels 51’)
KUNDI C:
Qarabag FK 0 - 0 Atletico Madrid
Chelsea 3 - 3 Roma
KUNDI D:
Barcelona 3 - 1 Olympiacos (Dimitrios
Nikolaou 18’og, Lionel Messi 61’, Lucas Digne 64’, Dimitrios Nikolaou 90’)
Juventus 2 - 1 Sporting CP (Miralem
Pjanic 29’, Mario Mandzukic 84’,
Alex Sandro 12’OG)
0 Comment untuk "Chelsea wabanwa mbavu darajani, Man U,PSG,Barcelona wakaribia 16 Bora"