Hatimae kitendawili cha nani
kuirithi mikoba ya Mayanja ndani ya Simba Sc kimeshatatuliwa baada ya kumpa
mkataba mrudi Masuod Juma ambae alikuwa anakinoa kikosi cha Rayon Sports.
Akizungumza na waandishi wa habari
msemaji wa timu ya Simba Haji Manara amesema “Juma ni mzoefu wa soka la Afrika kwa
kucheza na kufundisha” aliendelea kusema “wakati wa uchezaji wake walishawahi
kucheza na mtanzania Peter Manyika ”.
Kocha huyo anasifika kwa soka la
nguvu na kasi ametua leo jijini Dar es salaam na ametambulishwa rasmi mbele ya
waandishi wa habari.
Wasifu wa kocha:
Djuma Masoud (alizaliwa Agosti 30, 1977)
amezichezea klabu za Prince Louis (2002), Rayon Sport (2003-2009) na Inter Star
(2010).
Pia, Manara alimtambulisha meneja mpya wa
klabu hiyo, Richard Robert ambaye anachukua nafasi ya Cosmas Kapinga aliyerejea
kwa mwajiri wake kuendelea na kazi yake ya udaktari.
0 Comment untuk "MRITHI WA MAYANJA HADHARANI NI MASOUD DJUMA RAIA WA BURUNDI"