Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya
Tanzania Taifa Stars, Salum Shabani Mayanga amewaita kikosini viungo Jonas
Mkude kutoka Simba na Mudathir Yahya wa Singida United.
Mkude na Mudathir wanachukuwa
nafasi za Erasto Nyoni na Muzamiru Yassin wote kutoka Simba ambao awali
walijumuishwa kwenye kikosi cha wachezaji 24 walioitwa na Mayanga.
Kocha Mayanga amelazimika kuwaondoa
kikosini Nyoni na Muzamiru baada ya taarifa ya ufafanuzi kutoka Shirikisho la
Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kuhusiana na kadi nyekundu walizopata
wachezaji hao kwenye mchezo wa kirafiki uliopita.
Mchezo uliopita ulikuwa ni dhidi ya
timu ya The Flames ya Malawi uliomalizika kwa sare ya kufungana bao 1-1
uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa FIFA, Nyoni na
Muzamiru wataukosa mchezo ujao dhidi ya Benin kutokana na Kanuni za Nidhamu za
FIFA ambako kifungu cha 18 (4) kinaelekeza mchezaji mwenye kadi nyekundu
kuukosa mchezo unaofuata.
Kwa suala la mechi za kirafiki
kifungu cha 38 (2) (g), kinatamka wazi kuwa mchezaji mwenye adhabu ya kadi
nyekundu moja kwa moja anaukosa mchezo wa kirafiki unaofuata.
Kwa ufafanuzi huo wa FIFA, Mayanga
amewaondoa Nyoni na Muzamiru kikosini ili kutumikia adhabu hiyo kwa mchezo
unaofuata wa kirafiki na nafasi zao kujazwa na Mkude na Mudathir.
Wachezaji hao watajiunga kambini na
wachezaji wengine walioitwa katika kambi itakayoanza Novemba 5, mwaka huu
kujiandaa na mchezo huo wa kirafiki dhidi ya Benin utakaochezwa kwenye tarehe
za kwenye kalenda ya FIFA Novemba 12, huko Benin.
Wachezaji wengine wanaounda kikosi
hicho kinachodhaminiwa na Bia ya Serengeti ni
Makipa –
1.
Aishi Manula
2.
Ramadhani Kabwili
3.
Peter Manyika
Walinzi Wa Pembeni
4.
Gadiel Michael
5.
Boniphas Maganga
Walinzi Wa Kati
6.
Abdi Banda
7.
Kelvin Yondani
8.
Nurdin Chona
9. Dickson Job
Viungo Wa Kati
10. Himid Mao
11. Hamis Abdallah
12. Raphael Daudi
13. Mohamed Issa
Viungo Wa Pembeni
14. Simon Msuva
15. Shiza Kichuya
16. Faridi Mussa
17. Ibrahim Ajib
Washambuliaji
18. Mbwana Samatta
19. Mbaraka Yusuph
20. Elias Maguli
21. Yohana Mkomola
22. Abdul Mohamed
0 Comment untuk "Erasto Nyoni, Muzamiru Yassin Out, Jonas Mkude na Mudathir Yahya In Taifa Stars dhidi ya Benin"