Rekodi imevunjwa rasmi usiku wa
kuamkia leo ndani ya nchi ya Italia katika dimba la San Siro baada ya miaka 60
kupita.
Kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1958
taifa la Italia litakosa fainali za kombe la Dunia baada ya jana kukubali sare
ya 0 – 0 na Sweden hivyo Sweden kufuzu katika fainali za mwakani kwa ushindi wa
mchezo wa awali katika dimba la Friends
Arena ambapo walishinda goli 1 – 0 goli likifungwa na Jakob Johansson umbali wa
Yard 20.
Hii ina maana kocha Giampiero
Ventura ameshindwa kuipeleka Italia kwenye fainali hizo hivyo kuvunja mwiko wa
italia kutawala kwenye fainali hizo.
Nahodha wa Italia huenda akastaafu
michezo ya kimataifa baada ya mchezo wa jana usiku.
0 Comment untuk "HABARI PICHA NA UCHAMBUZI ITALIA IKITOLEWA NA SWEDEN KOMBE LA DUNIA 2018, NDANI YA SAN SIRO"