Msemaji wa timu ya Majimaji ya mjini
songea bwana Onesmo ameiambia Jamii fm ya Mjini Mtwara kuwa njia ya
kuwaunganisha mashabiki wa Majimaji ambao wamekata tama ni moja tu na ni
Ushindi pekee.
Bwana Onesmo alisema “unajua timu
yetu haijashinda hata mchezo mmoja, tumeongea na wachezaji na tumekubaliana ni
lazima tupambane kufa na kupona ili tupate pointi 3 na kufikisha pointi 8”
“Ukitazama timu yetu ni nzuri sana
ila lakini wachezaji walitueleza problems zao, tumekaa tumekubaliana na
tumedhamiria kushinda ili kurudisha morali kwa timu na mashabiki”alisema Onesmo
Mechi ya leo ni kati ya Majimaji vs
Stand United itapigwa kwenye dimba la Majimaji mjini Songea.
Timu zote mbili zipo mkiani wakati Majimaji
ikiwa imecheza michezo 8 na kuambulia pointi 5 katika nafasi ya 14.
Stand UTD wao pia wana pointi 5
katika nafasi ya 15 baada ya michezo 8
0 Comment untuk "Ligi kuu Tanzania bara kuendelea leo, Majimaji waapa kuingamiza Stand UTD"