Siku ya jumatatu mchezaji mwenye thamani kubwa Duniani
amesaini mkataba wa kuitumikia Real Madrid kwa kipindi kingine cha miaka 5,
mkataba ambao utamfanya awe ndie mchezaji anaelipwa pesa
nyingi zaidi $88m (80 million euros, £71 million) kwa mujibu wa American
magazine Forbes.
“Ninachokitaka ni kuendelea kufurahia miaka iliyosalia
kucheza, Nna miaka kumi (10) mbele ya kucheza”ni maneno ya Ronaldo baada ya
kusaini mkataba huo.
“mwaka huu ndio mwaka niliokuwa nauwaza kiukweli nimetimiza
ndoto zangu nimeshinda mataji mawili taji la ulaya, mabingwa ulaya na kusaini
mkata huu”
Ronaldo mwenye goli 371 katika mechi 360 tangu ajiunge na
Real Madrid 2009, pia amefanikiwa kuchukua kombe la ligi ya mabingwa mara mbili,taji
moja la laliga na mataji mawili ya kombe la ligi.
Wachezaji wengine wanategemewa kusaini mikataba na miamba
hiyo ya soka ni Gareth Bale, Luka Modric na Toni Kroos
Millionaire Ads
0 Comment untuk "CHRISTIANO RONALDO ASAINI MIAKA MITANO MADRID"