Sadio Mane akifunga mara mbili , Emre Can, Philippe
Coutinho, Roberto Firmino na Wijnaldum wote wakifunga mara moja na kuifanya
Liverpool kuibwaga Watford 6 – 1 katika dimba la Anfield.
“kama kuna mtu anazani kuwa mbele kwa pointi moja baada ya
mechi 11 tunatwaa kombe msimu huu, siwezi kumuelewa mtu huyo ” hayo ni maneno
ya Klopp
“kitu cha msingi ni kuhakikisha tunafikiria mechi
zilizobaki, ni mengi yatatokea wiki chache zijazo au miezi ijayo tunatakiwa
kuangalia kwa makini”
Wadau na mashabiki wa Liverpool wanaamini kuwa watavunja
mwiko wa miaka zaidi ya 26 ya ligi kuu kwa kubeba kombe hilo tangu walipolitwaa
mwaka 1990.
Millionaire Ads
0 Comment untuk "LIVEPOOL TULIENI SAFARI BADO NI NDEFU MANENO YA KLOPP"