Millionaire  Ads

Serengeti Boys yashinda rufaa, yafuzu mataifa Afrika U17

                                                         Serengeti Boys
CAIRO
Ni furaha ndermo na vifijo kwa watanzania wote na afrika mashariki yote baada ya shirikisho la soka Afrika(CAF) kupitia kamati yake tendaji  kuipa ushindi timu ya taifa ya vijana serengeti Boys katika kesi ya kupinga umri wa kijeba wa timu ya U17 ya Congo Brazzaville Langa-Lesse Bercy.


Langa-Lesse Bercy

Akizungumza na TBC waziri wa michezo Mh Nape Nnauye alisema Serengeti Boys wameshinda rufaa yao na hivyo watashiriki Mataifa ya Afrika mapema mwaka huu huko Madagascar.

Ikumbukwe srengeti boys ilitolewa na Congo kwa faida ya goli la ugenini, mchezo uliofanyika Dar es salaam boys waliitandika Congo 3-2 na mchezo wa marudiano Congo waliibuka na ushindi wa 1- 0.

Timu ya Serengeti ipo kwenye mawindo makali kwa ajili ya maandalizi ya michuano hiyo katika Uwanja wa karume zilipo ofisi za TFF


Millionaire  Ads

Share :

Facebook Twitter Google+ Lintasme
0 Comment untuk "Serengeti Boys yashinda rufaa, yafuzu mataifa Afrika U17"

Back To Top