Timu ya Azam leo Asbuhi imeondoka Kuelekea Swaziland tayari
kwa mchezo wa marudiano na Mbabane
Swallows.
Katika mchezo uliofanyika Tarehe 12 uwanja wa Chamanzi Azam
waliibuka na ushindi wa goli 1 kwa 0 kwa goli la Ramadhani Singano.
Azam wanaenda Swaziland kutafuta sare au ushindi wa aina
yoyote ile ili waweze kusonga mbele katika michuano hiyo ya kombe la shirikisho
barani Afrika.
Mchezo huo wa marudiano utafanyika jumapili ya 19 katika Uwanja
wa Somhlolo, mjini Mbabane.
Kocha Msaidizi wa timu ya Azam amewaondoa hofu watanzania
kwa kusema yafuatayo ““Maandalizi yako vizuri vijana wote wanafuraha, wanaari
na morali ya kuhahakisha tunasonga mbele katika raundi inayofuata, tunaenda na
changamoto kadhaa, ya kwanza kuhahakisha wavu wetu hautikiswi, kama hatufungi
basi tusifungwe,”.
Cheche aliendelea kusema “Tutaenda kufanya kazi ya uhakika,
lakini huku nyumbani tunawaomba Watanzania watuombee dua na vilevile waendelee
kutusapoti na sisi tutahakikisha tunawawakilisha vema ili kuipa hadhi nchi
yetu,”
Mungu ibariki Azam
Mungu ibariki Tanzania
Millionaire Ads
0 Comment untuk "Azam yaifuata Mbabane Swallows kwa matumaini kibao"