Maajabu ya soka
yametokea jana usiku baada ya PSG kukubali kipigo kitakatifu cha goli 6 – 1 nyumbani
kwa Barcelona.
PSG walihitaji sare au
kufungwa goli zisizozidi tatu ili kuweza kutinga hatua ya roba fainali ya ligi
ya mabingwa Kutokana na ushindi walioupata February 14, wa goli 4 – 0.
Mchezo wa jana ulianza
kwa wenyeji kujipatia goli ndani ya dakika tatu lililofungwa na Luis Suarez
baada ya mlinzi wa PSG Marquinhos kukosea kuokoa mpira uliopigwa na Rafinha na
kutua kwenye kichwa cha Suarez.
Dakika ya 40 Layvin
Kurzawa alijikuta akiipatia Barcelona goli la pili akiwa anajaribu kuokoa mpira
ulipigwa Kuelekea golini na Andres Iniesta,
Mpaka mapumziko
Barcelona 2 – 0 PSG
Dakika 48 Thomas
Meunier alimkwatua Neymar na mwamuzi wa mchezo huo aliamuru ipigwe penati,
penati ilipigwa na Lionel Messi na kuipatia timu yake goli la 3.
Mpira uliochongwa na Marco
Verratti ulitua kichwani mwa Layvin Kurzawa nae aliuunganisha hadi kwa Edson Cavani
ambae aliipatia PSG goli mnamo dakika ya 62.
88’ Neymar alifunga
kwa uhodari mkubwa adhabu ya moja kwa moja na kuipatia Barca goli la 4, dakika
2 badae Marquinhos alimfanyia madhambi Suarez kwenye eneo la penati na
kuamuriwa ipigwe penati ambayo ilifungwa tena na Neymar na kuipa timu yake goli
la 5.
Dakika 90+5 Sergi
Roberto scores aliibuka shujaa wa mchezo baada ya kuipatia Barca goli muhimu
sana na la kukumbukwa kufuatia kazi nzuri iliyofanywa na Neymar.
Hadi mwisho wa mchezo
Barcelona 6 – 1 PSG, hivyo Barcelona
wamesonga mbele kwa jumla ya magoli 6 – 5.
Millionaire Ads
0 Comment untuk "BARCELONA 6 - 1 PSG, historia yaandikwa ligi ya mabingwa Ulaya"