Kikosi cha yanga leo
kimeendelea na mazoezi makali kujiandaa na mchezo wa kilabu bingwa barani
Afrika hatua ya 32 dhidi ya Zanaco FC, ya Zambia siku ya jumamosi.
Jambo la kutia moyo
kwa wawakilishi hao wa Tanzania ni kurejea kwa nyota wa Yanga ambao walikuwa
majeruhi.
"tunaendelea na
mazoezi yetu na tunamshukuru Mwenyenzi Mungu baadhi ya wachezaji wetu waliokuwa
majeruhi ambao ni Ngoma Kamusoko na Tambwe tayari wamerejea na kuanza mazoezi
na kikosi,kiujumla wachezaji wote wana umhimu kwenye kikosi cha Yanga SC hivyo
kwa yeyote ambaye atatumika kwa upande wetu ni sawa na hakuna tatizo." Hayo
ni maneno ya Juma Mwambusi.
Mungu ibariki Yanga.
Mungu ibariki
Tanzania.
Millionaire Ads
0 Comment untuk "Ngoma, Tambwe, Niyonzima, Kamusoko fit kuwavaa Zanaco FC, ya Zambia"