Mkubwa mkubwa tu hatimae Ureno ya
Ronaldo na Argentina ya Messi ndani ya kombe la Dunia mwakani
Hatimae Lionel Messi ameweza kuibeba
timu yake ya taifa na kuipeleka fainali za mwakani za kombe la Dunia baada ya
jana kuifungia magoli muhimu matatu.
Messi alifunga magoli hayo dakika za
11,18 na 62 na kuifanya Argentina kuifunga Ecuador 3 – 1.
Kwa Matokeo hayo ya ushindi wa jana
yanaifanya Argentina kushika nafasi ya 3 kwa kujikusanyia jumla ya pointi 28 nyuma ya vinara Brazil
wenye pointi 41 na Uruguay wenye point 31
Kwa upande mwingine Ureno ya Ronaldo
imefanikiwa kuongoza kundi B baada ya ushindi wa goli 2 – 0 dhidi ya waliokuwa
vinara wa kundi hilo Switzerland.
Kwa mantiki hiyo Ureno wamefungana
pointi na timu ya Switzerland kila timu ina pointi 27 isipokuwa Ureno wao
wanamtaji mkubwa wa magoli ya kufunga na kufungwa.
Ureno wamefunga magoli 32 na
kufungwa 4 huku Switzerland ikiwa imefunga magoli 23 na kufungwa 7.
Ukiangalia takwimu hapo Ureno anautofauti
wa magoli 28 wakati hasimu wake huyo ana utofauti wa magoli 16.
Magoli ya Ureno yalifungwa na Johan
Djourou alijifungwa kwenye dakika ya 41 na goli la pili lilifungwa na Andre
Silva dakika ya 57
0 Comment untuk "Mkubwa mkubwa tu hatimae Ureno ya Ronaldo na Argentina ya Messi ndani ya kombe la Dunia mwakani nchini Urusi"