Mchezaji tegemeo kwa sasa kwa timu
ya Liverpool msenegal Sadio Mane atakaa nje kwa muda wa wiki 6.
Hii inatokana na kuumia katika
mchezo wa kufuzu kwa fainali za kombe la Dunia kati ya Senegal na Cape Verde.
Tukio hilo lilitokea dakika ya 89 na
kumfanya mchezaji huyo kutolewa nje.
Katika mchezo huo Senegal ilishinda
goli 2 – 0 kwa magoli ya Diafra Sakho 81', Cheikh Ndoye 90'.
Kwa mantiki hiyo Mane ataukosa
mchezo muhimu kati ya Manchester United na Liverpool mchezo wa ligi kuu nchini
England wikiendi hii.
Millionaire Ads
0 Comment untuk "SADIO MANE NJE WIKI 6,KUUKOSA MCHEZO WA LIVERPOOL DHIDI YA MANCHESTER UNITED WIKIENDI HII"