Timu ya Ndanda ya mkoani mtwara
imewakana wazamini wake wawili kampuni ya kiboko na Maxcom Lmtd.
Hayo yameibuka baada ya wadau kuanza
kuushutumu uongozi kuwa timu inalia ukata wakati timu ina wazamini wane.
George Njooka ambae ni katibu mkuu
wa timu ya Ndanda amesema wadhamini wanaowatambua ni Azam Tv na Vodacom na ndio
wanaotoa fedha ndani ya timu hiyo.
Aliwazungumzia kiboko “Kiboko yupo
anaitwa mdhamini kwa maana ya kwamba kile kipindi ambacho timu ya Ndanda kuna
wenzetu walitoka Dar es salaam wakawa wanataka kuungana na sisi kuendesha timu
na sisi tuliwakaribisha kuendesha timu wao kabla mamboyote hayajakaa vizuri
wakatafta wadhamini wakaenda kusaini mkataba na kiboko lakini utaratibu wetu
timu ya Ndanda inaongozwa na bodi ya wakurugenzi ” alisema Njooka.
Nae mwekahazina wa Ndanda amekiri
kupokea fedha toka kwa Azam Tv na Vodacom tu na hajapokea fedha nyingine
yoyote.
Millionaire Ads
0 Comment untuk "NDANDA YAWAKANA WAZAMINI NA KUONDOA MABANGO YAO UWANJANI"