Hali ya ukata ndani ya kilabu ya Yanga imeingia sura mpya baada ya
mkurugenzi wa ufundi wa timu hiyo kuachisha kazi rasmi leo.
Alipohojiwa Hans Van Pluijm alisema ““Nimepewa barua asubuhi hii
na yanga juu ya mkataba wangu kuwa umesitishwa, kikubwa walichokisema ni kuwa
klabu kwa sasa inakabiliwa na ukata hivyo hawana uwezo wa kuendelea kunilipa”.
Aliongeza kusema “Kwa sasa nipo huru kujiunga na klabu yeyote
itakayoonyesha nia na mimi basi nitafanya nao kazi”
Hans Van Pluijm amekuwa Kocha wa YAnga na amedumu tangu 2014–2016
na amefanikiwa kuifikisha timu hiyo katika hatua ya makundi kombe la washindi barani
Afrika msimu wa 2015/2016 kabla ya hivi karibuni kuja kwa kocha Lwandamina na
kufanya yeye kuwa mkurugenzi wa ufundi.
0 Comment untuk "BREAKING NEWS: Hans Van Pluijm afungashiwa virago yanga."