Jana usiku Mtanzania Mbwana
Samatta aliiwezesha timu
yake ya KRC GENK kuibuka na ushindi
kwa kupachika goli mbili katika dimba lao la nyumbani la Luminus Arena katika mchezo wa Ligi Kuu Ubelgiji dhidi ya vinara wa Ligi hiyo Club Brugge.
Mbwana Samatta dakika ya 5 alikokota mpira toka
katikati ya Uwanja baada ya kupokea pasi toka kwa Malinovsky na kuipa GENK goli la
kuongoza kabla ya kufunga la pili akitokea upande wa kushoto baada ya pasi ya Alejandro Pozuelo katika dakika 42, dakika
moja badae Brugge walipata goli la kufutia machozi lililofungwa
na Izquierdo dakika ya 43.
Matokeo
hayo yanaifanya KRC GENK kuendelea kuwa nafasi ya nane katika
msimamo wa Ligi Kuu Ubelgiji wakiwa na point 45,baada ya michezo 29 wakati Club Brugge wao wakiendelea kuongoza Ligi hiyo
inayoshirikisha timu 16 kwa kuwa na jumla ya point 58 sawa na Anderlecht waliyo nafasi ya pili baada ya
michezo 29.
Millionaire Ads
0 Comment untuk "Samatta apiga mbili Genk ikiifunga Club Brugge 2- 1"