Chelsea na Manchester tangu mwaka
2007 wamekutana mara 3 katika michuano ya kombe la FA na Chelsea kushinda mara
2 na kutoka sare mara 1.
19 May 2007 timu
hizi mbili zilikutana katika mchezo wa fainali kombe la FA katika dimba la
Wembley na Chelsea kutwaa kombe hilo
kwa kuifunga Manchester United goli 1
kwa 0 goli la Didier Drogba katika
dakika ya 116.
Goli hilo Drogber alilifunga baada
ya kuunganisha kwa kichwa mpira ulipigwa na Frank Lampard na kumshinda mlinda
mlango wa Manchester Edwin Van Der Sar.
Ikumbukwe Uwanja wa Wembley ndio
ilikuwa mara ya kwanza kuchezewa fainali za FA hivyo Chelsea kuandika rekodi ya
kuwa timu ya kwanza kutwaa ubingwa katika dimba hilo ikishuhudiwa na Washabiki 89,826.
Tarehe 10 Mar 2013 timu hizo
zilikutana katika Uwanja wa Old Trafford huku Washabiki 75,196 wakiwa uwanjani,
timu hizo zilitoka sare ya 2 – 2 katika mchezo wa raundi ya 6.
Magoli ya Manchester yalifungwa na Javier Hernandez dakika
ya 5 na Wayne Rooney dakika ya 11, magoli ya Chelsea katika mchezo huo
yalifungwa na Eden Hazard dakika ya 59, Ramires dakika 68.
Mwaka huo huo
walirudiana Tarehe 1 Apr na Chelsea walifanikiwa kuingia raundi ya 5 baada ya
kuifunga Manchester goli 1 kwa 0 katika dimba la Demba Ba dakika ya 49.
Leo Chelsea v Manchester United zinakutana katika hatua ya
robo fainali wakati huu ambao Chelsea inashiriki makombe mawili EPL na FA na Manchester inashiriki makombe
matatu EPL, FA na Europa na tayari wamehifadhi kombe moja.
Habari njema kwa Chelsea ni kuwa wachezaji wake 99% wako
salama na hivyo wako katika ari nzuri ya kushinda mchezo wa leo ukilinganisha
na Manchester ambayo wachezaji wake muhimu ni majeruhi, wachezaji majeruhi ni Wayne
Rooney na Anthony Martial wakati Marcus
Rashford akiwa ana ugua. Zlatan Ibrahimovic yeyeamepewa adhabu na chama cha
soka nchini Uingereza.
vikosi vinatabiriwa kuwa hivi
0 Comment untuk "Chelsea vs Manchester United, historia na utabiri na vikosi vya leo "