Kocha Mkuu wa timu ya mpira wa miguu ya Tanzania ‘Taifa Stars’,
Salum Mayanga leo Jumatatu Machi 13, 2017 ametangaza majina ya wachezaji 26
watakaounda kikosi cha timu ya Taifa.
Katika mkutano wake na wanahabari uliofanyika leo Makao Makuu ya
TFF, yalioko Uwanja wa Karume, Ilala jijini Dar es Salaam, Mayanga aliwataja
wachezaji hao kuwa ni walinda milango, Aishi Manula (Azam FC), Deogratius
Munishi (Yanga SC) na Said Mohammed (Mtibwa Sugar).
Walinzi wa pembeni upande wa kulia aliwataja Shomari
Kapombe (Azam FC) na Hassan Kessy (Yanga SC) wakati upande wa
kushoto wapo Mohammed Hussein (Simba) na Gadiel Michael (Azam FC).
Mayanga aliwataja walinzi wa kati Vicent Andrew (Yanga SC),
Salim Mbonde (Mtibwa Sugar), Abdi Banda (Simba SC) na Erasto Nyoni
(Azam FC) ilihali aliwataja viungo wa kuzuia kuwa ni Himid
Mao (Azam FC) na Jonas Mkude (Simba SC).
Kadhalika wako viungo wa kushambulia Salum Abubakar (Azam FC),
Said Ndemla (Simba SC), Frank Domoyo (Azam FC) na Muzamil Yassin (Simba)
wakati viungo wa kulia waliotajwa ni Simon Msuva (Yanga SC) na Shizza
Kichuya (Simba SC).
Viungo wa kushoto ni Farid Mussa (Teneriffe, Hispania) na Hassan
Kabunda (Mwadui FC) wakati washambuliaji ni Mbwana
Samatta (KRC Genk- Ubelgiji), Thomas
Ulimwengu na AFC Eskilstuna – Sweden), Ibrahim
Ajib (Simba SC), Mbaraka Yusufu(Kagera Sugar) na Abdul-Rahman Mussa (Ruvu
Shooting).
Pia Mayanga aliwataja wasaidizi wake kuwa Kocha Wa Makipa,
Patrick Mwangata wakati Meneja wa timu upande wa ufundi atakuwa mwenyewe
Mayanga na upande wa mipango mingine atakuwa Danny Msangi; Mtunza Vifaa, Ally
Ruvu wakati Daktari wa timuatakuwa Richard Yomba huku Daktari wa
viungo akiwa ni Gilbert Kigadya.
Taifa Stars, inatarajiwa kucheza na Botswana Machi 25, 2017
kabla ya kuivaa Burundi Machi 28, mwaka huu katika michezo kirafiki wakati huu
wa Kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).
Timu hiyo itaingia kambini Machi 19, 2017 kwenye Hoteli ya Urban
Rose, Dar es Salaam na mara baada ya michezo hiyo kambi itaahirishwa Machi 29,
mwaka huu.
Taarifa hii ni kwa msaada wa Website ya TFF
Millionaire Ads
0 Comment untuk "Kocha Mkuu wa timu ya mpira wa miguu ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Salum Mayanga atangaza kikosi "