Taifa Stars ya Tanzania kesho Machi
28, 2017 saa 10:00 jioni inaingia tena Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, kucheza
na Intamba Murugamba ya Burundi katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa, kwa
mujibu wa kalenda ya wiki ya mechi za kimataifa ya FIFA.
Huu ni mchezo wa pili kwa Taifa
Stars kucheza ndani ya wiki moja baada ya ule wa awali dhidi ya The Zebras
‘Pundamilia’ wa Botswana uliofanyika Uwanja huo wa Taifa, jijini Dar es Salaam
Jumamosi iliyopita na taifa stars kuibuka na ushindi wa 2 – 0
Source TFF
Millionaire Ads
0 Comment untuk "Kesho ni Stars na Burundi, je Stars kuendelea kutupa raha"