Wakati zikiwa zimebakia siku 4 jumamosi April 1, kwa mchezo unaosubiriwa kwa
hamu kati ya mabingwa wa ligi kuu Tanzania timu ya Yanga na mabingwa wa Afrika
mashariki na kati timu ya Azam habari
njema ni kupona kwa wachezaji muhimu wa timu hizo.
Kwa upande wa Azam ukuta wake
uliondokewa na beki wake kisiki Aggrey Morris, Morris alipata majeraha hayo
wakati Azam FC ikiichapa Mbabane Swallows bao 1-0 katika mchezo wa kwanza wa
Kombe la Shirikisho Afrika, ambapo katikati ya wiki iliyopita alianza programu
ya mazoezi ya ‘gym’ kabla ya leo kuhamia uwanjani.
Kwa upande mwingine kilabu ya Yanga
ambayo ilipata wakati mgumu wa kucheza na Zanaco bila kuwa na washambuliaji wa
kati, leo mchezaji tegemeo kwa ufungaji Amis Tambwe ameanza rasmi kujifua
uwanjani baada ya kupona majeraha yake.
0 Comment untuk "Tambwe wa Yanga Morris wa Azam fit kwa pambanano lao la April 1"