Millionaire  Ads

Azam vs Ndanda April 5, Yanga vs Prisons April 22 robo fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup)


Ratiba ya kombe la shirikisho Azam confederation Cup kati ya Azam na Ndanda toka mkoani mtwara katika hatua ya robo fainali sasa kupigwa April 5 Chamanzi Complex saa moja usiku.

Awali mchezo huo ulipangwa kufanyika kati ya Machi 18 na 19 mwaka huu, lakini ulisogezwa mbele kutokana na Azam FC kuwa kwenye majukumu ya mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Mbabane Swallows ya Swaziland ambapo Azam alitolewa kwa jumla ya 3 -1.

Mbali na mechi hiyo ya Azam FC, mtanange mwingine uliobakia utafanyika Aprili 22 mwaka huu kati ya mabingwa watetezi Yanga na Tanzania Prisons, utakaofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.


Mshindi wa michuano hiyo iliyorejea msimu uliopita, anatarajia kujishindia kombe pamoja na kitita cha Sh. milioni 50 na kuiwakilisha Tanzania Bara kwenye Kombe la Shirikisho Afrika mwakani.
Millionaire  Ads

Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comment untuk "Azam vs Ndanda April 5, Yanga vs Prisons April 22 robo fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup)"

Back To Top