Refa pekee kutoka Tanzania ambae
ameteuliwa na shirikisho la mpira wa miguu duniani kuchezesha fainali za kombe
la dunia kwa wanawake mwaka 2019 huko Ufaransa ndie muamuzi mchezo kati ya Azam
na Yanga.
Ikumbukwe kuwa zinapokutana mara
nyingi timu hizi mbili mchezo huwa mgumu na wenye hisia tofauti kwa waamuzi.
Tff wamempa jukumu mwanadada Jonesia
Rukyaa jukumu la kushika firimbi kuamua mchezo huo ambao ni muhimu kwa kila
timu.
Ikumbukwe kuwa mwanadada huyo amewahi kuchezesha michuano ya
Mataifa ya Afrika kwa wanawake iliyofanyika Cameroon mwaka jana na kuwa mwamuzi
wa kwanza wa kike nchini kuchezesha michuano hiyo mikubwa barani Afrika
Rukyaa amewahi kuchezesha mchezo
kati ya Yanga na Simba mtani jembeambapo simba waliibuka washindi kwa 3 - , pia mchezo Yanga na Simba mchezo wa raundi ya
pili ligi kuu Tanzania Bara ambapo Yanga walishinda 2 – 0.
Katika michezo hiyo hakujakuwa na
malalamiko hivyo Tff huenda wakamchagua Yeye Kutokana na uzoefu alionao kwa
michezo yenye msisimko kwa wadau wengi wa soka.
Millionaire Ads
0 Comment untuk "Refa wa kombe la duniani kuchezesha mechi ya Yanga na Azam jumamosi april 1"