
Timu ya Everton jana rasmi imeweza
kuitoa Manchester United katika nafasi yake ya 6 ambayo imedumu nayo kwa muda
mrefu sana.
Ushindi wa Everton wa goli 4 kwa 0 dhidi ya Hull City umeifanya Everton
kufikisha pointi 50 sawasawa na Arsenal angalia Msimamo upo chini na kukaa
katika nafasi ya 6.
Everton wamecheza michezo mitatu zaidi
ya Manchester United na miwili zaidi ya Arsenal na kutumia michezo hiyo kuipiku
United na kuikuta Arsenal.
Ushindi huo ambao ulitokana na
magoli mawili ya Romelu Lukaku ndani ya dakika 1 na Dominic Calvert-Lewin 9’ na
Enner Valencia 78’.
Wakati huohuo timu ya Arsenal
imekubali kipigo cha goli 3 – 1 dhidi ya West Bromwich Albion katika mchezo wa mapema
jana.
Matokeo hayo yameamsha upia Msimamo wa
mashabiki wakutaka kocha wao Arsenal
Wenger afukuzwe kwa kuwa ameshindwa kufanya kile wadau wanapenda.
Matokeo yote ya jana ni kama
ifuatavyo:
West Bromwich Albion 3 - 1 Arsenal
Stoke City 1 - 2 Chelsea
West Ham United 2 - 3 Leicester City
Crystal Palace 1 - 0 Watford
Everton 4 - 0 Hull City
Sunderland 0 - 0 Burnley
AFC Bournemouth 2 - 0 Swansea City
Michezo ya leo jumapili
Middlesbrough VS Manchester United 15:00
Tottenham Hotspur VS Southampton 17:15
Manchester City VS Liverpool 19:30
Msimamo wa EPL baada ya michezo ya jana
0 Comment untuk "Matokeo, Ratiba na Msimamo wa ligi kuu ya England, Arsenal hali tete, Leicester waendelea kujiimarisha, Everton waipiku Man U"