Ratiba hiyo iliyotelewa mapema leo imepangwa kama ifuatvyo:
March 18 Madini fc wataikaribisha Simba Sc katika dimba la Sheikh
Amri Abeid, Arusha, siku hiyohiyo ya Tarehe march 18 Kagera Sugar itaialika
Mbao ndani ya Uwanja wa Kaitaba, mjini Bukoba.
Michezo miwili iliyobaki ni kati ya Azam FC watakapoikaribisha
Ndanda fc toka Mtwara katika dimba la chamanzi.
Yanga wataikaribisha Tanzania Prisons katika Uwanja wa Taifa
jijini Dar es salaam.
Michezo kati ya Azam na Ndanda, Yanga na Prisons
haijapangiwa ni lini itafanyika Kutokana na Yanga kushiriki michuano ya kilabu
bingwa barani Afrika huku Azam wao wakishiriki michuano ya kombe la shirikisho
barani Afrika.
Mshindi wa michuano hiyo kikanuni anatarajia kujishindia
kombe pamoja na kitita cha Sh. milioni 50 na kuiwakilisha Tanzania Bara kwenye
Kombe la Shirikisho Afrika mwakani.
Madini vs Simba
Kagera vs Mbao
Yanga vs Prisons
Azam vs Ndanda
Millionaire Ads
0 Comment untuk " Ratiba robo fainali Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) imetolewa leo na michezo miwili kupigwa march 18."