Timu ya taifa ya Tanzania Taifa
Stars leo inaikaribisha timu ya Taifa ya Botswana katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa
ambao upo katika kalenda ya FIFA.
Wachezaji wanaocheza soka nje nchi
wameitwa ili kuhakikisha timu yetu inapata Matokeo chanya ili ipate alama
katika shirikisho la mpira wa miguu duniani na shirikisho la mpira wa miguu
Afrika ambapo Tanzania ipo chini sana ukilinganisha na Botswana.
Mchezaji kiongozi wa timu hiyo
Mtanzania anaekipiga huko ubeligiji katika timu ya Genk amerekodiwa na vyombo
vya habari akisema yafuatayo Kuelekea katika
mchezo huo
“Ni kweli katika timu ya taifa
kunahitajika uzoefu lakini ukiangalia kwa muda ambao Tanzania imekuwa
ikishiriki mashindano nafikiri bado hatujakuwa katika nafasi nzuri pamoja na
kuwa tulikuwa na wachezaji wazoefu lakini bado hatukuweza kufanikiwa kwa vile
tulivyokuwa tunataka tumpe nafasi kocha ya kufanya anachotaka”
Kocha wa timu ya Taifa Mayanga
amesema anaamini timu yake itafanya vizuri katika mchezo wa leo.
Viingilio vimepunguzwa ili
watanzania wote wenye nia ya kuuona mchezo huo waweze kujitokeza kuipa hamasa
timu yao.
Viingilio ni kama vifuatavyo:
Mzunguko sh 3000 badala ya sh 5000/=
VIP A sh 15,000/=
VIP B na C sh 10,000/=
0 Comment untuk "Stars mguu sawa kuivaa Botswana, TFF yapunguza viingilio"