Wakiwa wanaamini mpira umeisha Real Madrid walijikuta wakilowa mbele ya mashabiki wake 81044 katika dimba lao la Estadio Santiago Bernabeu kwa goli 3 kwa mbili.
Shujaa wa mchezo huu alikuwa ni
muagentina Lionel Messi ambae alifanya anavyotaka uwanjani huku hasimu wake
mkuu Ronaldo akiwa haonekani.
Kadi ya njano ndani ya dakika ya 12
kwa Casemiro baada ya kumkwatua Lionel Messi ilimfanya mbazili huyo kucheza kwa
tahadhari sana kuepuka kadi nyekundu.
Madrid ndio walikuwa wa kwanza
kupata goli mnamo dakika ya 28 kupitia kwa kiungo Mbrazil Casemiro ambae
aliunganisha mpira uliopigwa na Bale huku wachezaji wa Barcelona wakizani
ameotea.
Dakika ya 33 Rakitic alimpigia pasi
Messi akiwa ndani ya 18 nae bila ajizi alimpiga chenga Carvajal na kuukwamisha
mpira wavuni na kufanya Matokeo kusomeka 1 – 1.
Kipindi cha pili dakika ya 73 Ivan
Rakitic alifunga goli zuri kwa kuupeleka mpira upande wa kulia wa goli na
kuifanya Barcelona kuwa mbele kwa goli 2.
Madrid walicharuka baada ya tukio
hilo na kuliandama goli la Barcelona lakini uhodari wa Marc-Andre ter Stegen
uliwakosesha goli.
Mchezaji alieingia akitokea benchi
82’ James Rodriguez aliunganisha vizuri mpira uliopigwa na Marcelo na kuipatia
Real goli la pili mnamo dakika ya 86.
Dakika za nyongeza ndio ambazo
Madrid hawata kaa wazisahau milele pale walipofanya shambulio langoni mwa
Barcelona na kupokonywa mpira na Sergi Roberto aliekimbia nao kutoka nyuma ya
mstari wa katikati mpaka kwenye 18 ya Real upande wa kushoto na kupiga pasi
murua kwa Alba ambae alimuachia Messi na kuipatia timu yake goli la 3.
Kitu kizuri kwa messi leo n kuikisha
magoli 500 akiitumikia Barcelona
Kwa Matokeo hayo Barcelona
wanaongoza ligi kuu ya Hispania kwa tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa.
Barcelona imefunga magoli 94 na
kufungwa 32 hivyo tofauti ni 62
Madrid imefunga magoli 84 na
kufungwa 36 hivyo tofauti ni 48
0 Comment untuk "Muosha Huoshwa, Real Madrid 2 - 3 Barcelona ndani ya Estadio Santiago Bernabeu"