![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgO-D2cC9MlKFlQRFL6u8gdqzAnT7JhARF4WP_8NLtvMObX4pio6DaGwuvskcKlCIHCprr8D5aDSu3iZiG2PS16dpMRBz7YXNEvcmVDsAOvD27boNTRYJ_duLWBqJ7QdqzINEvnmt9EOHU/s640/str.jpg)
Leo usiku majira ya saa nne usiku
majogoo wa London timu ya Liverpool itakuwa ugenini kutafuta alama tatu muhimu
na kuendelea kujikita katika nafasi ya nne ambapo jana timu za jiji la Manchester
zilishindwa kuindosha Liverpool baada ya kukubali kupoteza alama mbili kila
timu.
Lallana amefanya mazoezi na kikosi
cha kwanza baada ya kukaa nje kwa muda wa mwezi mmoja Kutokana na majeruhi
yaliyokuwa yanamkabili.
Kwa sasa Liverpool na Manchester
City wanapointi sawa 66ila Liverpool inauwiano mzuri wa magoli ya kufunga na
kufungwa katika michezo 34.
Wakati Liverpool wakifurahia kurudi
kwa Lallana na Daniel Sturridge Watford wao watakosa huduma ya beki wao Craig
Cathcart ambae ana matatizo ya nyonga, pia itawakosa Younes Kaboul, Roberto Pereyra na mshambuliaji wao Mauro Zarate.
Kwa upande wa Liverpool itawakosa Jordan
Henderson, Sadio Mane, Ragnar Klavan na Danny
Ings.
Kocha wa Liverpool amenukuliwa na
SKY Sport akisema anaiamini timu yake na kila mmoja kwenye timu yake anania ya
kubaki nne bora ‘BIG 4’
kama una tangazo lako tafadhali tuwasiliane ili tukutangazie kwa bei nafuu kabisa, DMrutu ni kwa ajili ya watu wote, karibuni sana
0 Comment untuk "Daniel Sturridge na Adam Lallana ‘fit’ kuwavaa Watford leo jumatatu,"