Baada ya kutoa kipigo kizito kwa
mabingwa wa Africa chini ya miaka 17 wa mwaka 2003 cha goli 4 – 0 kocha Paa
Kwesi Fabin amesema anachoangalia yeye ni ushindi tu kwa kila timu atakayokutana
nayo na sivinginevyo aliiambia CAFonline.
mchezo huo utapigwa saa mbili nusu kwa saa za afrika mashariki.
Timu ya Gabon ndiyo mwenyeji wa
michuano ya mwaka huu lakini katika mchezo wake wa kwanza ilikubali kichapo cha
goli 5 – 1 kutoka kwa timu ya Taifa ya Guinea U17.
Mchezo wa leo Gabon watakuwa
wanahitaji ushindi kwa njia yoyote ili kujisafishia njia ya kucheza nusu
fainali, wakati Ghana wao wakishinda leo tayari watakuwa washatinga katika
hatua ya nusu fainali.
Timu zitakazofika hatua ya
nusufainali zote zitapata tiketi ya kucheza kombe la dunia nchini india badae
mwaka huu.
Ratiba ya leo na Msimamo wa kundi A,
angalia chini hapo:
Millionaire Ads
0 Comment untuk "Ghana vs Gabon, Kocha wa timu ya taifa ya Ghana U17 (Black Starlets) Paa Kwesi Fabin ameapa kutoionea huruma Gabon katika mchezo wake wa leo."