Unaweza kusema mzee Wenger atacheza
michezo miwili katika siku moja nikimainisha atacheza mchezo wake huku akiomba Liverpool
itoke sare au ifungwe ili yeye na timu yake waingie katika nafasi ya 4 ili
kuweza kupata nafasi ya kushiriki ligi ya mabingwa hatua ya mtoano.
Jana usiku
Arsenal walipata ushindi wa goli 2 – 0 dhidi ya Sunderland
Ila kwa timu itakayoshika nafasi ya
nne itabidi tena iombe dua mbaya kwa Manchester United ifungwe katika Fainali
ya Europa ili nafasi ya nne iwe salama kinyume cha hapo itabidi timu
itakayoshika nafasi ya nne ishiriki Europa.
Manchester City yenyewe ni
imejihakikishia kushika nafasi ya tatu au ya nne baada ya jana kuishindilia
timu ya West Bromwich Albion kwa goli 3 – 1 na kujisfikishia jumla pointi 75
ambazo Arsenal anaweza kufika ila City anauwiano mkubwa sana wa goli ya kufunga
na kufungwa 36, wakati Arsenal ina uwiano wa magoli 31, ili Arsena iweze kuitoa
City kwenye nafasi yake anahitajika ashinde goli zisizopungua 6 huku akiiombea
City ipoteze.
Hivyo tunaweza kusema Hesabu za
Wenger zimesalia kwa Liverpool pekee.
Millionaire Ads
0 Comment untuk " Hesabu za Arsene Wenger zimebaki kwa Liverpool pekee"