Timu ya Taifa ya MaliU17 jana usiku
imetetea kombe lake na kuingia kwenye historia ya Afrika.
Haikuwa kazi rahisi kwa Mali
kunyakua taji hilo kwani Ghana ilijipanga vilivyo, shukurani za pekee zimwende
mlinda mlango wa Ghana kwa kuinusuru timu yake na fedheha ya fainali baada ya
kuokoa penati mbili.
Mali walipata bao hilo la pekee
kupitia kwa Seme Camara na kunyakua ubingwa huo.
Mali ilikuwa kundi B Pamoja na
Tanzania ambapo walifuzu nusu fainali baada ya kuwa vinara kwa kujikusanyia
pointi 7, walitoka sare mchezo mmoja tu katika mashindano haya yote dhidi ya
Tanzania pekee.
Millionaire Ads
0 Comment untuk "Mali mabingwa AfrikaU17 mara mbili mfululizo yaifunga Ghana 1 – 0 mchezo wa fainali"