Hatimae mwenyezi Mungu amemjalia
uzima na afya kiungo mwenye mapafu mithili ya mbwa Jonas Mkude na kuruhusiwa
kutoka hospitali alipokua kalazwa na kujiunga na timu ya taifa tayari kwa
maandalizi ya michuano ya kufuzu Afrika.
Jana jumapili akitokea Dodoma gari
alilokuwa amepanda yeye na baadhi ya mashabiki wa Simba lilipinduka na
kusababisha kifo cha mpenzi wa simba Shose Fidelix (29) na kujeruhi wengine akiwemo
nyota huyo wa simba.
Taarifa tulizozipata kutoka kwenye
ukurasa wa simba ni kuwa marehemu Shose
msiba wake upo Mwembechai karibu na hoteli ya Itumbi.taarifa za mazishi
tutakujuza.
Mwenyezi Mungu awatie nguvu wapenzi,
wanachama wa simba na wadau wote wa soka katika msiba wa dada yetu Shose.
Millionaire Ads
0 Comment untuk "Jonas mkude aruhusiwa kutoka muhimbili ajiunga na kambi ya Stars"