Mara
baada ya michezo ya mwishoni mwa juma lililopita, Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania
Bara 2016/2017, inatarajiwa kuendelea Jumanne Mei 9, mwaka huu kwa mchezo mmoja
ambako Mabingwa watetezi wa Kombe hilo, Young Africans itaikaribisha Kagera
Sugar katika mchezo utakaofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia
saa 10.00 jioni.
Kwa mujibu wa ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom, mechi nyingine
mbili zitachezwa Ijumaa Mei 12, 2017 ambako Simba SC itaialika Stand United FC
ya Shinyanga kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati Azam FC siku hiyo
hiyo ya Mei 12, mwaka huu itakuwa mwenyeji wa Toto Africans ya Mwanza kwenye
Uwanja wa Azam ulioko Chamazi, Dar es Salaam.
Jumamosi Mei 13, mwaka huu JKT Ruvu itakuwa nyumbani Uwanja wa
Mkwakwani jijini Tanga kucheza na Majimaji ya Songea wakati Tanzania Prisons
itaikaribisha Ndanda ya Mtwara kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya ilihali
Mwadui ya Shinyanga itakuwa mgeni wa Mtibwa Sugar Uwanja wa Manungu ulioko
Mvomero, Morogoro huku Mbeya City ikisafiri hadi Dar es Salaam kucheza na Young
Africans kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Siku ya Jumapili Mei 14, mwaka huu African Lyon ya Dar es Salaam
itacheza na Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam ilihali siku
inayofuata, Jumanne Mei 16, mwaka huu Young Africans tena itakuwa mwenyeji wa
Toto Africans kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Funga dimba la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara itakuwa Mei 20,
mwaka huu kwa timu zote kucheza ambako Azam FC itakuwa mwenyeji wa Kagera Sugar
kwenye Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam wakati Majimaji itamaliza na Mbeya City
kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea wakati Simba na Mwadui zitacheza Uwanja
wa Taifa, Dar es Salaam.
Siku hiyo Mbao FC itaialika Young Africans ya Dar es Salaam
kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza wakati Stand United itamaliza na Ruvu
Shooting ya Pwani kwenye Uwanja Kambarage mjini Shinyanga ilihali Mtibwa Sugar
itakuwa mwenyeji wa Toto Africans ya Mwanza kwenye Uwanja wa Manungu, Morogoro
wakati Africans Lyon ikiwa mgeni wa Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Sokoine
jijini Mbeya na Ndanda itamaliza na JKT Ruvu mjini Mtwara kwenye Uwanja wa
Nangwanda Sijaona
0 Comment untuk "Ratiba michezo ya ligi kuu Tanzania michezo iliyobaki icheki timu yako ufanye tathimini"