Endapo Real Madrid watashinda au
watatoa sare mchezo wao wa mwisho wa ligi kuu ya Hispania dhidi ya Malaga
watakuwa wametwaa kome la ligi hiyo hvyo basi kwa mujibu wa mkataba kipindi cha
manunuzi ya mchezaji Isco toka Malaga
kwenda Real Madrid kinasema endapo Isco ataisadia timu ya Madrid kutwaa ubngwa
wa Laliga basi Madrid watalipa €1.
Isco alisajiliwa na Real Madrid
mwaka 2013 kwa kiasi cha €27m, katika usajili huo kuna kipengele ambacho
kinasema endapo Madrid watatwaa kombe ndani ya miaka mitano ya ligi basi
itabidi wailipe Malaga €1.
Real Madrid inahitaji sare au Matokeo
mabaya kwa Barcelona ili iweze kutwaa ubingwa wa Laliga.
Real Madrid wana pointi 90
katika michezo 37 wakati Barcelona wao wana pointi 87 katika michezo 37.
Wakati huo huo mshambuliaji wa
Barcelona Lionel Messi 98% ndio atanyakua kiatu cha mfungaji bora wa
ligi kuu ya Hispania.
Messi amefunga magoli 35 msimu huu
katika michezo 33aliyocheza, huku akiwaacha mbali Suarez mwenye goli 28 katika
michezo 34 na Ronaldo mwenye goli 24 katika michezo 28.
0 Comment untuk "Real Madrid wakishinda jumapili Malaga kulamba €1,Messi 98% mfungaji bora Laliga"