Tuzo za ligi kuu tanzania bara kwa mujibu ya tovuti ya TFF ni kama ifuatavyo:
Kamati Maalum iliyoundwa
kusimamia tuzo hiyo imefanya mabadiliko kiasi kwa kuongeza baadhi ya tuzo
ambazo hazikuwepo msimu uliopita lengo ikiwa ni kuboresha tuzo.
Tuzo zilizoongezwa ni:Tuzo ya
Heshima (ambayo itatolewa kwa mwanasoka nguli wa zamani mwenye historia nzuri
kwa soka la Tanzania).
Nyingine ni: Tuzo ya Kikosi
Bora cha Msimu (Itatolewa kwa wachezaji Bora 11 wa Ligi Kuu (VPL XI 2016/2017)
walioteuliwa kutokana na ufanisi wao katika ligi hiyo msimu huu.
Pia imeongezwa Tuzo ya Mchezaji
Bora mwenye chini ya umri wa miaka 20 (Hii itatolewa kwa wachezaji waliofanya
vizuri katika ligi ya vijana ya timu za Ligi Kuu ya Vodacom .
Tuzo hiyo ya Mchezaji Bora wa
Ligi ya Vijana itajulikana kama Tuzo ya Ismail Khalfan ikiwa ni heshima ya
kumbukumbu ya mchezaji Ismail Khalfan wa Mbao FC aliyefia uwanjani katika
mashindano hayo yaliyofanyika mkoani Kagera.
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF)
limefikiria kutoa tuzo hiyo kama njia mojawapo ya kuonesha kuthamini kipaji cha
mchezaji huyi wakati wa uhai wake.
Kutokana na mabadiliko hayo tuzo
zitakazotolewa katika sherehe hizo pamoja na Tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu
ya VPL ambayo ndiyo tuzo kuu, pia ni Bingwa wa Ligi Kuu, Mshindi wa Pili,
Mshindi wa Tatu, Mshindi wa Nne na Mfungaji Bora.
Nyingine ni Mchezaji Bora wa Ligi
Kuu, Golikipa Bora, Kocha Bora, Mwamuzi Bora, Mchezaji Bora wa Heshima,
Mchezaji Bia anayechipukia, Goli Bora la Msimu, Mchezaji Bora wa Kigeni,
Mchezaji Bora wa Chini ya Umri wa Miaka 20 na Timu Yenye Nidhamu.
Tuzo za Bingwa, mshindi wa pili,
wa tatu na wa nne na Mfungaji Bora hizi zipo kulingana na msimamo wa ligi
ulivyo.
Hata hivyo Mfungaji Bora safari
hii kuna wachezaji wawili wamefungana, hivyo kamati itapitia vigezo vilivyopo
katika Kanuni za kumpata Mfungaji Bora w Ligi Kuu Tanzania Bara ili kupata
mshindi ambaye atatangazwa siku hiyo ukumbini.
Wafuatao wameteuliwa kuwania tuzo
hizo kutokana na vigezo mbalimbali:
Mchezaji Bora wa Ligi Kuu
Aishi MANULA - Azam
Simon MSUVA - Yanga
Shiza KICHUYA - Simba
Haruna NIYONZIMA - Yanga
Mohammed HUSSEIN – Simba
(Majina ya wanaowania tuzo hiyo
yalitolewa Jumatano iliyopita na upigaji kura unaendelea ukiwahusisha Makocha
wa timu za Ligi Kuu na Makocha Wasaidizi,Wahariri wa habari za michezo na
Manahodha wa timu za Ligi Kuu, ambapo mwisho wa kufanya hivyo ni Jumanne Mei 23
mwaka huu).
KIPA BORA
Aishi MANULA - Azam
Owen CHAIMA - Mbeya City
Juma KASEJA - Kagera Sugar
KOCHA BORA
Joseph OMOG - Simba
Mecky MEXIME - Kagera Sugar
Ettiene NDAYIRAGIJE - Mbao
MWAMUZI BORA
Shomari LAWI – Kigoma
Elly SASII – Dar es Salaam
Hance MABENA - Tanga
MCHEZAJI BORA WA KIGENI
Haruna NIYONZIMA - Yanga
Method MWANJALE - Simba
Yusuph NDIKUMANA - Mbao
MCHEZAJI BORA ANAYECHIPUKIA
Mbaraka ABEID - Kagera Sugar
Shaaban IDD - Azam
Mohammed ISSA - Mtibwa
TUZO YA ISMAIL KHALFAN – (U-20)
Shaaban IDD - Azam
Abdalah MASOUD - Azam
Mosses KITAMBI - Simba
TUZO YA HESHIMA
(Atatangazwa aliyeteuliwa siku
hiyohiyo ya sherehe za tuzo).
GOLI BORA LA MSIMU
(Tayari yamepatikana mabao bora
10 ambayo yataoneshwa siku hiyo ukumbini ikiwemo lile bora la msimu mzima).
TIMU YENYE NIDHAMU
(Mshindi atatangazwa ukumbini
siku hiyo kulingana na vigezo vilivyopo).
WACHEZAJI 11 BORA WA MSIMU – VPL
XI 2016/17
(Watatangazwa ukumbini siku hiyo
ya sherehe).
Kamati inayohusika na usimamizi
wa tuzo inawaomba wadau wote ambao wameombwa kupiga kura katika Tuzo ya
Mchezaji Bora wafanye hivyo kulingana na fomu walizotumiwa na mchango wao una
thamani kubwa.
source:http://www.tff.or.tz/news/885-tuzo-za-ligi-kuu-2016-17
Millionaire Ads
0 Comment untuk "Sherehe za Tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inatarajiwa kufanyika Leo Mei 24,2017 ukumbi wa Mlimani City Dar es Salaam."